Tuesday, July 22, 2014

Tetesi za usajili barani Ulaya leo July 22 '14

Beki tegemezi wa Germany na Dortmund, Mats Hummels yupo kwenye hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Man utd. Taarifa kutoka Dailymail zinasema Hummels anaweza kujiunga na United ndani ya wiki hii. Tayari Ed Woodward ameshaondoka nchini Marekani ambapo Man utd wamepiga kambi na kurudi London ili kukamilisha usajili wa Hummels. 

Purchase: Mario Balotelli and his girlfriend Fanny Neguesha do some shopping in the Puma store
Balotelli ameendelea kuishinikiza klabu yake kumuuza kwenda Arsenal baada ya kupost picha akiwa mbele ya logo za Arsenal. Taarifa za Dailysports zinasema Ac Milan wameshakubali kumuuza mchezaji huyu na kwasasa yanaendelea mazungumzo kati ya wakala wa Balotelli na klabu ya Arsenal baada ya mchezaji huyu kutaka kulipwa paundi mil 5 kwa mwaka. 

Beki wa Holland na Ajax, Blind ameanza kuhusishwa na usajili kwenda Barcelona. Barca wameanza kumnyemelea beki huyu baada ya Valencia kuweka dau kubwa kwa Jérémy Mathieu. Kwasasa Blind yupo jijini Barcelona kwa mapumziko sambamba na kuharakisha usajili wake kwenda Barca. 

The Mirror limesema klabu ya Chelsea itatangaza muda wowote wiki hii usajili wa Didier Drogba. Mchezaji huyu anayechezea klabu ya Gala nchini Uturuki anatarajiwa kurudi darajani na kusaini mkataba wa mwaka mmoja. 

Gazeti la Italia, Sport ltalia linasema mshambuliaji wa PSG,  Edinson Cavani ameendelea kuishawishi klabu yake kumruhusu kujiunga na Man utd. Man utd ilishaonesha nia ya kumsajili mchezaji huyu lakini PSG bado wameweka ngumu hadi muda huu. 

Mfungaji bora wa kombe la dunia, James, ameshawasili jijini Madrid tayari kukamilisha usajili wake kutoka Monaco kwenda Real Madrid kwa Euro mil 75. 

View image on Twitter
Patrice Evra ameshajiunga na Juventus ya Italia baada ya kuitumikia Man utd kwa miaka nane na nusu. Evra amecheza jumla ya mechi 379 akiwa na Man utd na kufunga magoli 10. 

Wanted man: Manchester City and Liverpool could bid for Real Madrid midfielder Isco this summer
Dailymail linaripoti kuwa klabu ya Liverpool imetuma maombi kwa Real Madrid ili kumsajili Isco. Taarifa hizi zinasema Real Madrid watakuwa tayari kumuuza mchezaji huyu ili kuweza kukusanya pesa za kumsajili James anayetarajiwa kutua Madrid kwa paundi mil 60. Mbali ya Isco Liverpool wapo kwenye hatua za mwisho kumsajili beki za Southampton Dejan Lovren kwa paundi mil 20. Mchezaji huyu anaweza kutangazwa rasmi kujiunga na Liverpool ndani ya wiki hii. 

No comments:

Post a Comment