Saturday, August 9, 2014

Tetesi za usajili ulaya 9 Aug 14

the front MD aug 9 2014
Tayari magazeti mbalimbali ya England na Spain yamethibitisha usajiliwa wa Vermaelen kutoka Arsenal kwenda Barcelona kwa ada ya paundi mil 15. Gazeti la Mundo limesema Vermaelen anatarajiwa kwenda jijini Barcelona wikiendi hii ili kufanyiwa vipimo na kutangazwa rasmi. 

Proved performer: Mangala, left, celebrates scoring in the Europa League against Sevilla in April
Klabu ya Man city inatarajia kumtangaza Mangala kuwa mchezaji wake baada ya kukamilisha usajili wa paundi mil 32 kutoka Porto ya Ureno. 

Klabu ya Man utd ipo kwenye mkakati wa kumsajili beki wa Ajax na Uholanzi, Daley Blind. Mtandao wa Dailysport umeandika habari hizi kwa kusema, tayari klabu yake imeshamruhusu kuondoka na hata mazoezi hafanyi na wachezaji wenzake. Blind alishahusishwa na Barcelona, lakini usajili wa Vermaelen kwenda Barca unamfanya Blind awe huru kuelekea Man utd. 

On the move? The Colombian only joined Monaco last summer but he looks set to move yet again
Klabu ya Liverpool ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao kwa mkopo. Dailysport limesema, Liverpool ipo tayari kulipa paundi mil 10 ili kumnasa mshambuliaji huyu baada ya Remy kushindwa vipimo. Kikwazo kikubwa cha usajili wa mchezaji huyu kwenda Liverpool ni klabu ya Real Madrid ambayo pia inamhitaji. 

Daily Express linasema klabu ya Man utd imetuma maombi ya paundi mil 55 kwa klabu ya Real Madri ili kumsajili Di Maria. Maombi haya yamekuwa ya pili baada ya mara ya kwanza kukataliwa. Man utd na Real Madrid wanaweza kukubaliana kumsajili mchezaji huyu baada ya PSG kushindwa kufikiana dau na Madrid. 

Klabu ya Juventus na Man utd bado hazijafikiana makubaliano ya kumnunua Arturo Vidal, hivyo tetesi za usajili wa mchezaji huyu bado zinaendelea. 

Gazeti la Mirror limesema klabu ya Sevilla itamruhusu beki wake Alberto Moreno kujiunga na Liverpool baada ya mchezaji huyu kucheza mechi dhidi ya Real Madrid kwenye fainali za Super Cup jumanne ijayo. 

Mtandao wa Goal, umesema klabu ya Ajax ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili Samwel Eto'o. Taarifa hizi zimekuja baada ya mkurugenzi wa Ajax, Marc Overmars kuthibitisha kuongea na mchezaji huyu na kwamba Eto'o ameonesha nia ya kutaka kujiunga na Ajax. 

Marca limeripoti tetesi za Alex Song wa Barcelona kusakwa na Man utd. Marca limesema Man utd inamuhitaji Song baada ya usajili wa Vidal kuwa na vikwazo vingi. Song atakuwa ni chaguo zuri la bei poa kwa United kwani mchezaji huyu hayupo kwenye mipango ya kocha mpya wa Barca, Lucho. 

No comments:

Post a Comment