Klabu ya Fc Barcelona inatarajia kwenda China, Malaysia na
Thailand mwishoni mwa msimu kucheza mechi za kirafiki. Hii itakuwa ni mara ya kwanza
kwa Barcelona kwenda Malaysia na Thailand licha ya kuwa na wapenzi wengi.
Barcelona watakuwa China agosti 3, Thailand agosti 7 na Malaysia agosti 10.
Ikiwa nchini Malaysia Barcelona itacheza na timu ya taifa kwenye uwanja wa
Bukit Jalil jijini Kuala Lumpur na inakadiriwa watazamaji 100,000 wanatarajiwa
kuingia. Mbali ya mechi za kirafiki katika nchi hizi Barcelona pia itafanya
shughuli zingine za kijamii pamoja na utalii.
No comments:
Post a Comment