Wednesday, April 3, 2013

Tevez kafungiwa kuendesha gari UK


Carlos Tevez mshambuliaji wa Man City leo amehukumiwa kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya paundi 1,145 baada ya kushikwa na polisi akiendesha gari bila insurance. Carlos Tevez aliamua kulipa faini ya paundi 1,145 na kutumikia kifungo cha nje kwa kuhudumia jamii kwa masaa 250 ndani ya miezi 12 ijayo. Tevez pia hatoruhusiwa kuendesha gari kwa kipindi cha miezi sita na itamlazimu kupewa kibali na mahakama ili aweze kuendesha tena gari baada ya miezi sita kuisha. 

Tevez akiendeshwa na mpenzi wake wakitoka mahakamani

No comments:

Post a Comment