Saturday, October 5, 2013

Sanamu ya Zinadane na Materazzi yawekwa Qatar

New home: The statue has this week been unveiled in the Qatari capital of Doha
Hii ni sanamu inayomuonesha kiungo wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane akimpiga kichwa Marco Materazzi (Italy) kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani. Tukio hili la Zidane kumpiga kichwa Materazzi lilizua gumzo sana mwaka 2006 baada ya fainali hizi. Kila mtu alitaka kujua kwanini Zidane alimpiga kichwa Materazzi, lakini habari zilikuwa sio rasmi zilisema Materazzi alimtukuna Zidane kuhusu dada yake. Kutokana na historia ya tukio hili, taasisi ya masuala ya kihistoria nchini Qatar imechukua uamuzi wa kuweka sanamu hii ili iwe kumbukumbu ya tukio hilo na kivutio cha watalii kwenye mji huo wa Doha.  
Backdrop: Doha Corniche, overlooking the Gulf, will house the statue
Seeing red: Zidane plants his brow into Materazzi's chest
Tukio halisi la Zidane kumpiga kichwa Materazzi. Baada ya tukio hili Zidane alipewa kadi nyekundu. Italy ndiyo walioibuka washindi kwenye fainali hii kwa mikwaju ya penati 5 - 3. 

No comments:

Post a Comment