Saturday, May 11, 2013

FIFA yaionya Brazil kuhusu kombe la dunia 2014

Shirikisho la mpira duniani FIFA limetoa onyo kwa Brazil kuhusu ukamilikaji wa viwanja vitakavyotumika kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2014. FIFA imesema haitabadilisha msimamo wake wa kuitaka Brazil iwe imekamilisha viwanja vyote desemba mwaka huu 2013. Kauli hiyo ya FIFA imekuja kwasababu hadi sasa viwanja sita bado havijakamilika na mategemeo ya kukamilika ndani ya mwaka huu ni madogo. Viwanja ambavyo bado havijakamilika ni pamoja na Cuiaba, Manaus, Natal, Curitiba, Porto Alegre na Sao Paulo. Vilevile FIFA imesema viwanja vyote vinatakiwa kujaribishwa mara mbili vikiwa vimejaa watu kabla havijatumika kwenye kombe la dunia. Uwanja ambao ulikuwa kwenye matengenezo na kukamilika ni Maracana tu ambao ulizinduliwa mwezi wanne na ndiyo utakao tumika kwenye mechi ya fainali. Fainali za kombe la dunia zitaanza tarehe 2 mwezi Juni 2013 na zitafanyika kwenye miji 12 kama inavyoonekana kwenye ramani. 

No comments:

Post a Comment