Wednesday, June 5, 2013

Tatizo la Ronaldo anajifanya anajua sana - Mourinho

Kocha mpya wa Chelsea, Jose Mourinho ameamua kusema ukweli kuhusu mahusiano yake na Cristiano Ronaldo wakati alipokuwa Real Madrid. Mourinho akiongea na Intereconomia television ya Hispania aliulizwa kuhusu mahusiano yake na Cristiano na je atamshawishi ajiunge na Chelsea?, Mourinho alisema “Ronaldo hawezi kuja Chelsea na siwezi kumshawishi aje kwasababu mahusiano yetu yalishavunjika nilipokuwa Real Madrid, tatizo la Ronaldo anajifanya anajua kila kitu, haamini kama kocha anaweza kumfundisha mbinu ambazo zitamfanya awe bora zaidi, nilichokuwa namwambia alikuwa hatekelezi, anajiamini kuwa anajua zaidi yangu, binafsi sikuwa nafurahia tabia yake, hivyo mchezaji wa aina hii siwezi kumuita, labda uongozi wa Chelsea walazimishe aje kujiunga na sisi lakini sio kwa mahitaji yangu”. Lakini Mourinho alimalizia kwa kusema “Ronaldo ni mchezaji mzuri sana, hilo nalijua na nalikubali, lakini akiweza kujifunza kusikiliza ushauri wa kocha atakuwa bora zaidi”. Jose aliulizwa swali hili kutokana na tetesi zilizopo kuwa Ronaldo anataka kujiunga na Chelsea ili kumfuata Mourinho, lakini kulingana na majibu ya Mourinho basi ni wazi kuwa Ronaldo sio chaguo la Chelsea hadi sasa. 

No comments:

Post a Comment