Tuesday, July 16, 2013

Liverpool FC wapaa kuelekea Mashariki ya mbali

Liverpool players board the jet Liverpool's personalised jet
Wachezaji wa klabu ya Liverpool na viongozi leo wamepaa kuelekea kwenye ziara nchini za Mashariki ya mbali  kuanzia Indonesia kabla ya kuelekea Australia na Thailand. Jumla ya wachezaji 27 wamejumuishwa kwenye kikosi hicho akiwemo Luis Suarez. Ingawa Suarez hakuwepo kwenye kikosi kilichopanda ndege leo, klabu ya Liverpool imesema, Suarez pamoja na wenzake ambao bado wapo likizo watajiunga na wenzao hivi karibuni ndani ya ziara yao. Wachezaji wengine waliopo kwenye kikosi hicho ni Johnson, Enrique, Toure, Agger, Alberto, Gerrard, Aspas, Coutinho, Assaidi, Pacheco, Henderson, Downing, Spearing, Lucas, Mignolet, Allen, Borini, Sterling, Kelly, Skrtel, Flanagan, Wisdom, Robinson, Ibe, Coates, Reina.

You'll never fly alone: Liverpool's aeroplane had a familiar message on it
Ndege ya shirika la ndege la Indonesia ambao ni wadhamini wa usafiri wa klabu ya Liverpool ikiwa na nembo mbalimbali za klabu hiyo. Ndege hii ndiyo itatumika kuwasafirisha wachezaji wa Liverpool kwenda sehemu tofauti duniani ikiwemo kwenye ziara mashariki ya mbali kabla ya ligi kuanza.
Last on the plane was Steven Gerrrard Fabio remembered to bring his shades with him

No comments:

Post a Comment