Monday, October 14, 2013

Ghana kumkosa mchezaji muhimu dhidi ya Misri

Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Ghana, Kevin-Prince Boateng atakosa mechi ya mkondo wa kwanza ya kujitafutia nafasi kushiriki kombe la dunia dhidi ya Misri, kutokana na jeraha la goti. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alipata jeraha hilo kwenye mechi ya ligi wakati anaitumikia klabu yake Schalke. Majeraha haya yataifanya Ghana ikose mchango muhimu sana kutoka kwa Boateng kwani uwezo wake unatambulika. Ghana na Misri zinatarajiwa kushuka dimbani kesho (15 Octoba) mjini Kumasi Ghana. Mchezo huu ndiyo umetajwa kuwa mgumu kuliko yote kati ya mechi tano zinazokutanisha timu za Afrika kufuzu kombe la dunia. 

No comments:

Post a Comment