Monday, October 14, 2013

Safari ya Nigeria kombe la dunia imeiva

Roar of delight: Emmanuel Emenike (centre) celebrates after converting the winner from the spot
Ushindi wa Super Eagles ya Nigeria ugenini dhidi ya Ethiopia umeipa matumaini ya kushiriki kombe la dunia lijalo nchini Brazil. Ethiopia ilipata goli la kuongoza kunako dakika ya 56 kupitia Asefa. Bao hilo halikukaa kwa muda mrefu, kwani kunako dakika ya 67 mkwaju uliopigwa na Emanuel Emenike ulikwenda moja kwa moja nyavuni na kufanya matokeo yawe 1-1. Ethiopia watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi kadhaa walizopata na kama wangezitumia vyema matokeo yangeweza kuwa tofauti. Goli la ushindi la Nigeria limepatikana kwenye dakika ya mwisho kwa njia ya penati iliyofungwa na Emmanuel Emenike. Ushindi huu umeifanya Nigeria kujihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya kombe la dunia mwakani kwani itahitaji droo au ushindi wa aina yoyote kwenye mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa mwezi ujao. 

Matokeo ya mechi za Afrika

Burkina Faso 3-2 Algeria
Ivory Coast 3-1 Senegal
Ethiopia 1-2 Nigeria
Tunisia 0-0 Cameroon
Ghana vs Egypt (15 Oct 2013) 

In action: Samuel Eto'o turned out for Cameroon but drew a blank in a bore draw
Eto'o akipambana na mchezaji wa Tunisia katika mechi iliyokwisha kwa droo ya bila kufungana 

No comments:

Post a Comment