Wednesday, October 2, 2013

Goli la Ozil kuingia kwenye magoli bora ya msimu

Kiungo mpya wa Arsenal, Mesut Ozil ameendelea kung'arisha nyota yake akiwa na klabu ya Arsenal. Katika mechi ya jana usiku Uefa Champions dhidi ya Napoli, Ozil alicheza mpira safi uliovutia jambo ambalo limemfanya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kujisikia furaha kwa kuona mchezaji aliyemnunua kwa bei kubwa analeta faida zaidi ya pesa iliyotumika. Mbali ya kucheza vyema katika mechi ya jana, Ozil pia alifanikiwa kufunga goli zuri, goli ambalo linatarajiwa kuwa moja kati ya magoli bora kwenye michuano ya Uefa msimu huu. Kuthibitisha hili, magezeti karibia yote ya michezo nchini Uingereza na kwenye baadhi ya nchini yamepambwa na kicha za habari kikuu kuhusu Ozil na goli alilofunga. Chini ni baadhi ya picha na video kuhusu Mesut Ozil.


Magazeti ya Uingereza yalivyopendeza na jina la Ozil leo asubuhi 
What a finish: Ozil latched on to Aaron Ramsey's cross to side-foot the ball past Pepe Reina
Ozil akiangalia mpira alioupiga ukielekea nyavuni
Breakthrough: This graphic shows the move that gave Arsenal the lead, with Ozil (11) providing the finish
Ramani ya jinsi goli lilivyofungwa na Ozil 
Back of the net: The German playmaker's cool finish flies past the helpless former Liverpool goalkeeper

Video inayoonesha goli lilivyofungwa 

No comments:

Post a Comment