Wednesday, October 2, 2013

Liverpool yawarudisha Robbie, Steve na Rob

steve
Steve 
Klabu ya Liverpool imewarudisha tena wachezaji wake wa zamani Robbie Fowler, Steve McManaman na Rob Jones kuitumikia. Robbie, Steve na Rob wamepewa majukumu ya kuwafundisha wa watoto waliopo kwenye academy za klabu hiyo. Kurudi kwa wachezaji hawa ulikuwa ni mpango wa kocha wa sasa wa Liverpool, Brendan Rodgers wa kuimarisha vijana na watoto waliopo ndani ya klabu. Bredan Rodgers akiongelea jambo hili alisema ‘Ni furaha kuwa pamoja tena na Robbie, Steve na Rob. Nakumbuka mwishoni mwa msimu uliopita nilisema kuwa nitawaleta wachezaji wa zamani ili wajiunge nasi kwenye majukumu mbalimbali ya klabu. Hawa wachezaji ni muhimu sana kwa kuijenga klabu, kwasababu ndoto za vijana wetu ni kuwa kama wao, hivyo watafurahi kuwaona wakiwa pamoja. Tumeanza na hawa wachezaji watatu, naamini watawasaidia sana vijana wetu kujiendeleza katika soka kwa kuwafundisha jinsi wao walivyofanya wakafanikiwa’. Liverpool "You'll Never Walk Alone"     

Pride: Robbie Fowler and other Liverpool legends are mentoring young players at the club
Robbie Fowler alijiunga na Liverpool mwaka 1984, na hadi anastaafu mwaka 2001 alikuwa ameshacheza mechi 316 akiwa na Liverpool na aliweza kufunga magoli 128. 
Passion: Former midfielder Steve McManaman can teach young Reds to respect the shirt and the club's history
Steve McManaman alijiunga na Liverpool mwaka 1990 hadi 1999. Steve alicheza mechi 272 akiwa na Liverpool na alifanikiwa kufunga magoli 46. 

No comments:

Post a Comment