Friday, October 11, 2013

Wilshere kupigwa benchi kwasababu ya sigara

Magazeti mengi ya nchini England, leo yamepambwa na kichwa cha habari kuhusu Wilshere kupigwa benchi na kocha wa timu ya taifa kutokana na uvutaji wa sigara. Wilshere amekubwa na balaa hili baada ya kushikwa ndani ya klabu moja ya starehe wiki hii akivuta sigara wakati akijua haruhusiwi kufanya hivyo. Taarifa kutoka kwenye magazeti hayo zinasema, kocha wa England Roy, amefanya uamuzi huo ili kufundisha mchezaji huyu kuipenda afya yake na kutoa funzo kwa wengine. Kukosekana kwa Wilshere kwenye mechi ya leo kati ya England na Montenegro, kutamfanya Roy kuwatumia Gerrard, Lampard na Milner sehemu ya kiungo na washambuliaji watakuwa ni Rooney, Sturridge na Welback. 

No comments:

Post a Comment