Thursday, October 10, 2013

Majeraha ya Alonso chanzo ni nini????

Tokea msimu huu wa ligi uanze ni mwezi wa pili sasa, na Xabi Alonso bado hajapona majeraha ambayo yanasemekana yangeweza kuepukika. Alonso alianza kujisikia maumivu kwenye mguu wake wa kulia katikati ya msimu uliopita. Alitoa taarifa za kujisikia maumivu, lakini kutokana na ratiba ngumu iliyokuwepo kwa Real Madrid kwenye mechi za ligi na Uefa, Mourinho alimhitaji mchezaji huyu kuendelea kucheza huku akipatia matibabu madogo madogo. Hali hii, ilifanya majeraha aliyonayo kuzidi kuongezeka siku hadi siku. Baada ya msimu kuisha, madaktari wa klabu walimfanyia vipimo vya uhakika na kugundua mfupa wake wa kukanyagia kwenye mguu wa kulia umepata majeraha na ikabidi mchezaji huyu afanyiwe upasuaji mwezi Juni mwaka huu. Tokea mwezi Juni hadi leo hii, Alonso anatumia magongo kutembea ili kuwezesha sehemu aliyofanyiwa upasuaji kuunga vizuri. 

Kuwa nje kwa kipindi kirefu, kumeifanya klabu ya Real Madrid kuathirika kwa kiasi kikubwa, kwani hadi sasa nafasi yake kiwanjani bado haijapata mwenyewe aliyeweza kuiziba vilivyo. Alonso anatarajiwa kurudi dimbani kwa uhakika mwezi Novemba, licha ya kuwa dokta wa timu amesema kuna uwezekano mdogo wa kurudi mwishoni mwa mwezi huu Oktoba.  
Majera haya ya Xabi Alonso ambayo yangeweza kuepukika kama klabu ingekubali kumfanyia matitabu mara tu alipotoa taarifa, lakini uzembe huo umemfanya Alonso akose mechi nyingi zaidi za mwanzo wa ligi na pia utamfanya achelewe kujiunga na kikosi cha timu ya taifa kitakachokwenda Brazil. 

No comments:

Post a Comment