Monday, November 4, 2013

Mastraika 7 walio kwenye form msimu huu Ulaya

Diego Costa can't stop scoring (©GettyImages)
Diego Costa (Atletico Madrid) ligi ya Hispania, ameshacheza mechi 12 na anaongoza kwa ufungaji wa magoli ligi ya Hispania akiwa na jumla ya magoli 13. Mchezaji huyu amekuwa mwiba mkali kwa timu pinzani ndani ya ligi na kwenye michuano ya Uefa kwani takwimu zinaonesha Diego Costa ana uwiano wa kufunga goli moja katika kila mechi anayocheza. Kutokana na kiwango alichokionesha Diego Costa hadi sasa, kimefanya mahitaji yake kuongezeka kwani klabu kadhaa zimehusishwa kutaka kumsajili kwenye dirisha dogo ikiwemo Chelsea na Arsenal.  

Laying down his chips: Daniel Sturridge scored his side's fourth goal against the Baggies with a cute effort
Daniel Sturridge (Liverpool) ligi ya England, ameshacheza mechi 10 na amefanikiwa kufunga magoli 8 akiwa kileleni pamoja na Sergio Arguero. Sturridge ameweza kuonesha kiwango kizuri msimu huu kuliko msimu uliopita, jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa klabu ya Liverpool kuwa nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi kuu nchini England. 

In control: Striker Radamel Falcao shields the ball from Lyon's Maxime Gonalons during Monaco's 2-1 victory
 Radamel Falcao (Monaco) ligi ya Ufaransa, amefanikiwa kufunga magoli 8 akiwa nafasi ya pili ya ufungaji kwenye ligi ya Ufaransa nyuma ya mpinzani wake Edinson Cavani mwenye magoli 9. Falcao ameingia kwenye orodha hii kwasababu ya ugeni wake kwenye klabu ya Monaco na ameweza kuifungia klabu yake magoli ya ushindi kwenye mechi karibu zote ambazo Monaco imeshinda na kuifanya Monaco iendelee kung'ang'ania nafasi tatu za juu kwenye ligi ya Ufaransa. 

High earner: PSG's Zlatan Ibrahimovic will not be pleased about the proposed 75% tax on footballer's wages in Ligue 1
 Zlatan Ibrahimovic (PSG) ligi ya Ufaransa, tofauti na wengine, Ibrahimovic amevuma sana msimu huu kwenye michuano ya Uefa champions kuliko ligi ya nyumbani. Mchezaji huyu hadi sasa ana jumla ya magoli 6 kwenye michuano hiyo baada ya kufunga magoli manne kwenye mechi iliyopita. Katika kuthibitisha kiwango cha mchezaji huyu, Rais ya FIFA, Sepp Blatter mwezi huu alimtaja Ibrahimovic kuwa ni tishio kubwa kwa Ronaldo na Messi kwenye kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa dunia kutokana na kiwango chake cha juu alichokionesha kwenye klabu na timu ya taifa ya Sweden. 

Three and easy: Robert Lewandowski scored a hat-trick ahead of Borussia Dortmund's clash with Arsenal
Robert Lewandowski (Dortmund) ligi ya Ujerumani, ameshacheza mechi 11 na anaongoza kwa ufungaji wa magoli Ujerumani kwa kuwa na magoli 9. Mchezaji huyu uwezo wake unajulikana baada ya kufanya kweli katika msimu uliopita na kuiwezesha klabu yake kufika fainali ya Uefa champions na pia alikuwa mfungaji bora namba mbili wa michuano ya Uefa msimu uliopita akiwa na jumla ya magoli 10. Kiwango cha mchezaji huyu kimeendelea kuwavutia makocha wengi akiwemo Gurdiola, Wenger na Martino wa Barcelona. 

Giuseppe Rossi (Fiorentina) ligi ya Italia, ameshacheza mechi 11 na anaongoza kwa ufungaji wa magoli kwenye ligi ya Italia kwa kufunga magoli 9 hadi sasa. Rossi ametajwa kuwa moja kati ya washumbuaji bora msimu huu kutokana na ukweli kwamba, klabu yake ipo nafasi ya sita, lakini ameweza kuongoza kwenye ufungaji wa ligi ya Italia na kuwashinda washambuliaji wa klabu zile zinazoshikilia nafasi tatu za juu. 

Edinson Cavani (Ligi) ya Ufaransa, ndiye mchezaji anayeongoza kwa ufungaji wa magoli hadi sasa kwenye ligi ya nchini hiyo akiwa na jumla ya magoli 9 mbele ya washindani wake Ibrahimovic na Falcao. Cavani ambaye msimu huu ni wa kwanza akiwa na PSG, amefanikiwa kujihakikishia namba kwenye klabu yake baada ya kuonesha uwezo mkubwa wa kufunga magoli 9 katika mechi 12 alizocheza na pia ameweza kuonesha ushirikiano mzuri na Ibrahimovic, mchezaji ambaye ndiye supastaa wa PSG. 

No comments:

Post a Comment