Klabu ya Man utd imepoteza nafasi yake ya kwanza kama klabu
ya mpira wa miguu tajiri kuliko zote duniani na nafasi yake kuchukuliwa na Real
Madrid. Taarifa za Forbes wiki hii zinasema Man utd imekuwa namba moja toka mwaka 2004
lakini mwaka huu imeshuka kwa mara ya kwanza tokea Forbes waanze kuthaminisha
vilabu vya soka duniani. Real Madrid imeweza kuipiku United kwa kufikisha
mapato ya paundi bilioni 2.15 kwa mwaka, wakati Man utd wakiwa nafasi ya pili ambapo mapato yao ni paundi bilioni 2.07. Barcelona wanashika nafasi ya tatu wakifutiwa na
Arsenal nafasi ya nne wakati Bayern Munich wanashika nafasi ya tano.
Real
Madrid imeweza kuimarisha zaidi mapato yake kupitia mapato makubwa ya uwanjani,
hakimiliki za kuonesha mechi zake na matangazo mbalimbali ya ndani na nje ya
uwanja. Forbes imesema mbali ya Real Madrid kuizidi Man utd kwa tofauti ya
fedha chache lakini Real Madrid imeonekana bado ni imara zaidi kiuchumi
ikilinganishwa na United kwa kigezo kuwa imeweza kushika namba moja ikiwa bado
inaweza kuwalipa mishahara mikubwa wachezaji wake kama Cristiano, Kaka na kocha
wake Mourinho ambaye ndiye kocha anayelipwa zaidi ya makocha wote wa soka duniani
ambapo malipo yake kwa mwaka ni paundi milioni 12.3 tofauti na Sir Alex Ferguson
anayelipwa paundi milioni 7.6. Vilevile Real Madrid ndiyo klabu yenye historia ya kununua wachezaji kwa pesa nyingi kulizo zote duniani, ikikumbukwa uhamisho wa Cristiano Ronaldo wa dola milioni 80 ambao hadi leo ni rekodi ya dunia.
No comments:
Post a Comment