Thursday, January 2, 2014

Azam na Tusker zashinda Mapinduzi Cup

Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc wameanza vema michauano ya mwaka huu baada ya kuwachapa wenyeji, timu mseto ya Unguja (Spice Stars) kwa magoli 2-0 katikamchezo uliopigwa uwanja wa Amaan Zanzibar. Magoli ya Azam yalifungwa na Brian Umony aliyeingia kipindi cha pili kuchukjua nafasi ya mshambuliaji mpya rais wa Ivory Coast Mamadou Kone akiunganishga pasi murua ya chini kutoka kwa Kipre Bolou na la pili limewekwa kimiani na kiungo Himid Mao katika dakika ya 86 aliyeuwahi mpira uliotemwa na mlinda lango Silima aliyekuwa ajiribu kuzuia shuti la Salum Abubakar. 

Katika mchezo wa pili umeshuhudia makamu bingwa wa mwaka jana, Tusker ya Kenya wakipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ashanti United iliyochukua nafasi ya Yanga dakika za mwisho. kabla ya mashindano kuanza. Goli pekee lilifungwa na mshambuliaji Joishua Oyoo kwa mkwaju mkali akiwa ndani ya eneo la hatari baada ya walinzi wa Ashanti kuzubaa. Mchezo wa tatu kwa leo ulipigwa Gombani Pemba, timu mseto ya Pemba (Clove Stars) imekuwa ya kwanza miongoni mwa timu wenyeji kupata pointi katika mashindano ya mwaka huu baada ya kulazimishwa sare ya magoli 2-2 na URA ya Uganda.

No comments:

Post a Comment