Thursday, January 23, 2014

Tetesi za usajili barani Ulaya 24 Jan 14'

Mohamed Salah's deal to Chelsea is agreed
Klabu ya Chelsea imeipiku klabu ya Liverpool kwa kumsajili mshambuliaji wa FC Basel, Mohamed Salah kwa paundi mil 11. Mshambuliaji huyu tayari alikuwa kwenye hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Liverpool na alikwenda jijini Liverpool kukutana wa viongozi wa klabu ili kumalizia makubaliano. Makubaliano baina ya Liverpool na FC Basel yamechukua muda kutokana na kutokukubaliana kuhusu ada ya uhamisho. Klabu ya FC Basel ilikuwa ikihitaji paundi mil 12 wakati klabu ya Liverpool ilikuwa tayari kulipa paundi mil 5 hadi 8. Mvutano huu baina ya Liverpool na FC Basel ndiyo uliyoipa mwanya klabu ya Chelsea kumnasa Salah kutoka mikononi mwa Liverpool. Chelewa chelewa mtoto sio wako, poleni WanaLiverpool. 

Habari kutoka Dailysports zinasema tayari Juan Mata ameshatua kwenye kiwanja cha kufanyia mazoezi cha klabu ya Man utd kwa kutumia helikopta akitokea London. Mata anatarajiwa kufanyiwa vipimo na madaktari wa klabu ya Man utd kabla ya kusaini mkataba na kutambulishwa rasmi kwa mashabiki. Mata amesajiliwa na Man utd kwa paundi mil 37 na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne. 

Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger jana alikuwepo uwanjani kuangalia mechi kati ya Levante vs FC Barcelona mechi iliyokwisha kwa Barcelona kushinda magoli 4-1. Fununua kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na vyombo vya habari ni kwamba, Wenger alikwenda nchini Hispania kuwaangalia wachezaji watatu wa klabu ya Barcelona ambao ni Pedro, Reberto na Tello ili aweze kumsajili mmoja wapo. Wachezaji hawa watatu katika mchezo wa jana walionesha kiwango cha hali ya juu, jambo ambalo kwa namna yoyote lazima walimshawishi Wenger. Taarifa kamili za ziara ya Wenger zitajulikana hivi karibuni baada ya usajili utakapofanyika. 

Arsene Wenger aqui en una imag 54399443338 54115221154 600 396 Arsene Wenger & Ivan Gazidis were at Levante Barcelona watching Sergi Roberto & Cristian Tello [El Mundo Deportivo]


Baada ya klabu ya Man utd kumnyakua Juan Mata, klabu ya PSG imepata nguvu ya kuweza kumsajili Pogba na tayari klabu hiyo imetoa ofa ya paundi mil 70. Kabla ya United kumsajili Mata, klabu hizi mbili zilikuwa kwenye ushindani wa kumsajili kiungo huyu wa Juventus, lakini kwasasa mbio za kumsajili mchezaji huyu zimebakia kwa PSG. 

Television ya nchini Uingereza ITV sports imethibitisha kuwa klabu ya Real Madrid itatuma ofa ya paundi mil 25 kumsajili mshambuliaji wa Man utd Wayne Rooney. Ofa hii ya Madrid inatarajiwa kukubaliwa na klabu ya Man utd mwishoni mwa msimu huu. United imeshaonesha nia ya kumuuza Rooney baada ya kujiridhisha kuwa mchezaji huyu hataki tena kuichezea United. Jambo hili limethibitika baada Rooney kugoma kusaini mkataba mpya na United.  

 
The Sun linahabarisha kuwa klabu ya Arsenal imetoa ofa ya paundi mil 20 pamoja na Podolski ili kumsajili mshambuliaji wa Schalke, Julian Draxler. Ombi la Arsenal bado halijajibiwa licha ya kuwa uwezekano wa Draxler kuhamia Arsenal ni mkubwa. 
Gazeti la Marca linaripoti kuwa klabu ya Liverpool ipo kwenye mchakato wa kuzungumza na klabu ya Ac Milan ili kumsajili kiungo wake Nigel De Jong. Jong aliyejiunga na Ac Milan akitokea Man city ametajwa kuhamia Liverpool ili kuweza kuziba nafasi ya  Lucas Leiva ambaye ni majeruhi. 

No comments:

Post a Comment