Thursday, January 23, 2014

Neymar amfukuzisha kazi Rais wa Barcelona

Rais wa Barcelona aliyejiuzulu Sandro Rosell (kushoto) akikumbatiana na  Josep Maria Bartomeu, Makamu wa Rais ambaye atashika nafasi ya Urais kwasasa hadi hapo uchaguzi mwingine utakapofanyika. Rosell amechukua hatua hii ya kujiuzulu kufuatia tuhuma alizoletewa kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Barcelona, Neymar. Neymar aliyesajiliwa mwaka jana kutoka Santos ya Brazil, alitajwa kusajiliwa kwa ada ya Euro mil 57, lakini taarifa kutoka ndani ya klabu ya Barcelona zilisema Neymar alisajiliwa kwa Euro mil 95. Kutokana na kuvuja kwa siri hii ambayo Rosell ameshindwa kujitetea hadi kupelekea jambo hili kupelekwa mahakamani ndiyo sababu kubwa iliyomfanya ajiuzulu Urais wa klabu.  

Judge agrees to hear Neymar lawsuit
Neymar akiwa na Rosell wakati wa utambulisho 

No comments:

Post a Comment