Friday, January 3, 2014

Tetesi za usajili dirisha dogo leo 3 Jan 2014

Arsenal vs Berbatov
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekanusha vikali kuhusu tetesi zilizopo kuwa klabu yake ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Fulham Dimitar Berbatov. Wenger alisema ' hakuna jina la mchezaji ambalo tunaweza kulitaja ili kumsajili, hiyo itakuwa ni utovu wa nidhamu. Kwasasa wachezaji wote tuliyotaka kuwasajili kwenye safu ya ushambuliaji wapo kwenye mikataba mirefu na timu zao, hivyo tunachokifanya ni kuongeza juhudi za kuwaimarisha washambualiji tulio nao ili waweze kulingana na mahitaji yetu'. Washambuliaji wa klabu ya Arsenal kwasasa ni Nicklas Bendtner, Giroud na Lukas Podolski. 

Mata vs Chelsea 
Marginalised: Despite his impressive talent, Juan Mata is on the fringes at Chelsea
Baada ya kugombana na Mourinho, kiungo wa Chelsea Juan Mata bado hajafahamu mipango yake, kifupi yupo 50-50 kwani anaamini kuwa kiwango cha kucheza Chelsea bado anacho, ila hafahamu malengo ya kocha wake dhidi yake. Mata anaamini kuwa mfumo wa sasa anaotumia Mourinho ndiyo sababu yakucheza chini ya kiwango, tofauti na mfumo uliokuwa ukitumika msimu uliopita wa kucheza kwa nafasi. Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa Mata zinasema, mchezaji huyu bado hajafanya maamuzi ya kuondoka na iwezekana akaendelea kuwepo hadi mwisho wa msimu licha ya mahitaji yaliyopo kutoka kwa klabu za PSG, Tottenham, Inter Milan na Arsenal.  

Raheem Sterling vs Swansea
Klabu ya Swansea inamnyemelea kiungo wa Liverpool, Raheem Sterling ili kuweza kuimarisha kikosi chake. Klabu ya Swansea imepata hamasa ya kumsajili mchezaji huyu kwasababu ya kutokuwa nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza. Swansea iliyopo nafasi ya 13 ikiwa na tofauti ya pointi 7 tu kutoka timu ya mwisho, inahitaji kuongeza nguvu ya kutosha ili kuimarisha kikosi kuepukana na kushuka daraja.  

Chelsea vs Higuain 
Jose Mourinho amewaambia waandishi wa habari leo kuwa Higuain ni mchezaji mzuri, angependa kuwa naye lakini ana miezi sita tu tokea ahamie Napoli hivyo anaamini Napoli haiwezi kumuuza mchezaji huyu kwasasa.  

Barcelona/Bayern Munich vs Luiz 

Klabu za Bayern Munich na Barcelona bado hazijakata tamaa ya kumsajili beki wa Chelsea na Brazil, David Luiz. Beki huyu alikuwa kwenye hatua za mwisho kuhamia Barcelona mwanzoni mwa msimu, lakini Mourinho alizuia uhamisho huu mara tu baada ya kutua Chelsea akitokea Madrid. Luiz kwasasa hana namba ya uhakika kwenye kikosi cha Chelsea akipokezana nafasi na Terry au Cahill. Watu wa karibu na mchezaji huyu wanasema Luiz yupo tayari kuhama Chelsea lakini kocha Jose Mourinho amegoma kumuuza kwani bado anahitaji mchango wake kwenye safu ya ulinzi. 

Manchester United vs Reus 

Kiungo wa Borussia Dortmund Marco Reus amekanusha vikali na tetesi zilizopo kuwa atajiunga na Man utd ndani ya dirisha dogo. Reus amesisitiza jambo hili la kutohama ikiwa pia ni shinikizo kutoka kwa kocha wa klabu hiyo, kwani Reus ndiye kiungo mshambuliaji anayetegemewa na Dortmund. Ikumbukwe tu kwasasa Dortmund ipo nafasi ya nne kwenye ligi ikijikongoja kurudisha kiwango chake cha msimu uliopita na vilevile imeingia kwenye hatua ya 16 bora ya Uefa champions, Dortmund haipo kwenye kipindi kizuri cha kuweza kumruhusu mchezaji huyu kuondoka. 

No comments:

Post a Comment