Sunday, February 16, 2014

Azam FC yatolewa kwenye michuano ya Afrika

Wawakilishi wa Tanzania bara kwenye michuano ya Afrika klabu ya Azam FC leo imetolewa kwenye raundi ya kwanza baada ya kukubali kipigo cha magoli 2 -0 dhidi ya klabu ya Ferroviariao kutoka nchini Msumbiji. Katika mchezo uliyochezwa leo mjini  Beira, Azam ilitakiwa itoke droo au kufungwa kwa tofauti ya goli moja, kwani katika mchezo wa awali, klabu ya Azam ilishinda goli 1-0 jijini Dar es salaam. Kutokana na matokeo haya, Tanzania bara imebakiza mwakilishi mmoja kwenye michuano ya Afrika ambayo ni timu ya Yanga baada ya jana kushinda magoli 5-2 dhidi ya Wamoroco. 

Hawa ni Watanzania wanaoishi Msumbiji wamesafiri kutoka kutoka miji mbalimbali kushangilia timu ya nyumbani uzalendo wa kweli


No comments:

Post a Comment