Tuesday, February 25, 2014

Campbell kinda wa Arsenal aliyewaliza United

Arrival: Campbell slides on his knees in celebration of his goal just after half-time
Bila ya ubishi Joel Campbell muda wake wa kuchezea Olympiacos kwa mkopo utasitishwa mwisho mwa msimu huu na kurudi kikosi cha kwanza cha timu ya Arsenal. Uhakika wa mchezaji kurudi kwenye klabu yake ya Arsenal ni mkubwa baada ya kuonesha uwezo mzuri wa kumiliki mpira na kufanga kwenye mechi kati ya Olympiacos na Man utd. Campbell alikuwa akicheza kama kiungo mshambuliaji aliweza kuwatoka kirahisi mabeki wa Man utd, Vidic, Smalling na Ferdinand na kuifanya safu ya ulinzi wa Man utd kuwa kwenye hali tete kwa kipindi chote cha mchezo. Mchezaji huyu ambaye ni raia ya Costa Rica alijiunga na Arsenal mwaka 2011 akiwa na miaka 19 na ameshachezea klabu kadhaa kwa mkopo kabla ya kwenda Olympiacos. Hakika Arsene Wenger, ameshamuona na uwezekano wa kumrudisha kikosini msimu ujao ni mkubwa. 

Golazo: Campbell wheels away with his team-mates as Olympiacos took an unprecedented 2-0 lead

Dream come true: Campbell is paraded as an Arsenal player after signing in 2011 as a 19-year-old
Campbell siku alipojiunga na Arsenal mwaka 2011


No comments:

Post a Comment