Friday, April 25, 2014

Kocha wa zamani wa Barca afariki dunia

Vilanova
Kocha wa zamani wa Barcelona Tito Vilanova amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 45. Vilanova amefariki kwa maradhi ya kansa ya koo. Vilanova aliacha kazi ya kuifundisha Barcelona mwaka jana baada ya kuona afya yake sio nzuri, hivyo aliachia ngazi ili aweze kuendelea na matibabu. FC Barcelona watamkumbuka Vilanova kwa mengi ikizingatiwa kuwa yeye ndiye alikuwa msaidizi mkuu wa Pep Guardiola kocha ambaye ana historia ya kipekee ndani ya Barca. Vilanova pia aliiwezesha Barca kuendelea kuyaenzi mafunzo ya Guardiola baada ya kocha huyo kuhamia Bayern Munich. Tokea achukue timu Vilanova aliweza kushinda kombe la ligi mwaka 2013 na kuiwezesha Barca kufika nusu fainali ya Uefa champions. Wanamichezo mbalimbali Ulaya na duniani wameshaanza kutuma salamu za rambirambi wa familia ya Vilanova na Barcelona kwa ujumla. 

Juan Mata
Sergio Ramos
David De Gea
Samir Nasri
Success: Vilanova helped Barcelona lift their 22nd La Liga title in 2013
Gone, but not forgotten: Barcelona have said the club is in 'immense mourning'
Upset: Vilanova stepped down as manager at the start of this season and Gerardo Martino took over

No comments:

Post a Comment