Friday, July 19, 2013

Hatimaye Neymar kuvaa namba 11 Barcelona

Kulikuwa na kitendawili kikubwa kuhusu namba ambayo angeivaa mshambuliaji mpya wa Barcelona Neymar pindi atakapoanza kucheza kwani namba aliyokuwa akiivaa mchezaji huyu kwenye klabu ya Santos ni namba 11 na wakati anasajiliwa na Barcelona namba hiyo ilikuwa inavaliwa na Thiago Alacantara. Mbali ya kuwa namba 11 ilikuwa ikivaliwa na Thiago, vilevile namba zote kuanza 2 hadi 18 zilikuwa na wenyewe. Kufuatia hali hii klabu ya Barcelona ikabidi imtambulishe Neymar kwa mashabiki akiwa na jezi isiyokuwa na namba yoyote. Lakini baada ya Thiago kuuzwa kwenda Bayern Munich namba 11 imebakia wazi na hatimaye leo klabu ya Barcelona imetangaza rasmi kuwa Neymar atavaa namba 11 na tayari jezi zake zimeshawekwa kwenye maduka ya klabu hiyo na kuanza kuuzwa kwa kasi. 

Jezi za Neymar zikiwa kwenye duka la Barcelona, watu wameshaanza kuzichangamkia kwa kuzinunua kwa kasi

No comments:

Post a Comment