Sunday, May 18, 2014

Kocha wa Barcelona aachia ngazi

Kocha wa Klabu ya Barcelona, Tata Martino ametangaza kuachia ngazi baada ya kushindwa kunyakua kombe la ligi. Taarifa hii ameitoa leo baada ya Barcelona kutoka droo na Atl Madrid ya goli 1-1 na kuifanya Atl Madrid kuwa mabingwa wa ligi ya Hispania. Mkataba wa Tata ulikuwa na mashariti ya kushinda kombe la ligi na kufikia hatua ya nusu fainali au kunyakua kombe la ligi ya mabingwa Ulaya jambo ambalo ameshindwa kutimiza hivyo kutangaza kuachia ngazi. Tayari klabu ya Barcelona imekamilisha maongezi na kocha wa Celta Vigo, Luis Enrique ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Barca kuchukua mikoba ya Tata na muda wowote Enrique atatangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo. 

No comments:

Post a Comment