Wachezaji wanaogombania tuzo ya The Marc Vivien Foe wametangazwa leo na chombo cha habari France 24. Tuzo hizo za Marc Vivien Foe ni mahususi kwa kuchagua mchezaji bora wa Afrika anayecheza soka katika ligi ya Ufaransa. Tuzo ya Marc Vivien Foe imeanzishwa ili kumkumbuka Foe ambaye alikuwa mchezaji wa Olympique Lyon kabla ya kuanguka na kufariki akiwa uwanjani. France 24 imewatangaza wachezaji kumi na moja (11) wanaowania tuzo hii mwaka huu kuwa ni Aymen Abdennour (Tunisia, Toulouse) Kossi Agassa (Togo, Stade de Reims) Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon, Saint-Etienne) Andre Ayew (Ghana, Olympique Marseille) Foued Kadir (Algeria, Olympique Marseille) Wahbi Khazri (Tunisia, Bastia) Saber Khelifa (Tunisia, Evian) Nicolas Nkoulou (Cameroon, Olympique Marseille) Jonathan Pitroipa (Burkina Faso, Stade Rennais) Alaixys Romao (Togo, Olympique Marseille) Alain Traore (Burkina Faso, FC Lorient). Washindi wa miaka iliyopita, 2009 - Marouane Chamakh (Morocco, Bordeaux) 2010 – Gervinho (Ivory Coast, Lille – former club) 2011 - Gervinho (Ivory Coast, Lille – former club) 2012 - Younes Belhanda (Ivory Coast, Montpellier)
No comments:
Post a Comment