Azam FC yaichapa Prisons 3-0, Simba hoi kwa Kagera
Bocco, Mcha , Menowakimpongeza Tchetche wa Azam
Timu ya Azam FC imezidi kusonga mbele kwenye ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Tanzania Prisons 3-0 katika mchezo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi. Azam FC imepata ushindi huo wa nyumbani huku mshambuliaji wake Kipre Tchetche akijiweka katika nafasi nzuri yakutwaa kiatu cha dhahabu kwa kufikisha magoli 12 tofauti na wafungaji wengine kwenye ligi kuu. Wakati huo huo wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club leo wamepigwa goli moja kwa bila na Kagera Sugar mechi iliyofanyika Bukoba mjini na kuzidi kupoteza matumaini ya kutetea ubigwa. Kwa matokeo ya leo Azam inaendelea kushika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 40 wakati Simba ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi 34.
No comments:
Post a Comment