Yvette na Jordan |
Mkongwe wa kikapu, Michael Jordan anatarajiwa kufunga ndoa ya siri na Yvette Prieto tarehe 27
April mwaka huu. Katika taarifa zilizotolewa na “The Chicago Sun” zinasema watu
wengi maarufu nchini Marekani wamepewa kadi za mwaliko katika harusi hiyo
itakayofanyika kwenye bichi ya The Palm Fla nchini Marekani, lakini cha
kushangaza kwenye maelezo ya kadi hizo za mwaliko waalikwa wameambiwa
wasimjulishe mtu, vilevile hakuna mtu atakayeruhusiwa kuingia na simu, camera
wala kifaa chochote kitakachoweza kupiga piga, kuchukua video au sauti. Michael
Jordan katika ahadi yake na Yvette ni kuwa atamlipa dola za kimarekani milioni
moja kila mwaka na wakifika miaka kumi ataongeza malipo na kufikia dola milioni
tano. Mwaka 2006, Michael aliachana na mke wake Juanita Vanoy na kumlipa dola
milioni 168.
No comments:
Post a Comment