Friday, March 29, 2013

Chelsea tuna ratiba ngumu - Benitez


Kocha wa Chelsea Rafa Benitez amesema ratiba ya Chelsea wiki hii ni ngumu kutokana na mechi za ligi na FA kufuatana. Benitez alisema "jumamosi tunacheza na Southampton baada ya masaa 48 tunacheza na Man utd kwenye FA". Benitez aliongeza kwa kusema, “sisi tupo tofauti na wenzetu wa Man utd kwasababu Man utd hawana presha na ligi kuu kwahivyo watachezesha kikosi cha pili dhidi ya Sunderland, na kikosi cha kwanza kitapumzika kuja kucheza na sisi jumatatu, lakini sisi mechi zote mbili ni za muhimu sana, kwasababu kwenye ligi tunachuana na Spurs na Arsenal kutafuta nafasi ya UEFA na vilevile kombe la FA tunalihitaji ikiwa ndiyo kombe lililobakia kwetu”. Kwa mazingira haya lazima nichezeshe first eleven yangu kwenye mechi zote ikizingatia bado wachezaji wanauchovu baada ya kucheza kwenye mechi za kimataifa kuwania kombe la dunia. Hayo yalikuwa ni maneno yake RAFA BENITEZ kocha wa Chelsea. Kiukweli ligi ya BPL ipo patamu, mashabiki tunangojea kuona nini kitatokea. 

No comments:

Post a Comment