Kocha wa Man utd amedhibitisha kupona kwa wachezaji wake
watatu ambao ni Scholes, Jones na Nani. Sir Alex amesema wachezaji hao wamerudi
kwenye kipindi kizuri ili kuipa timu nguvu ya kupambana na Chelsea kwenye
FA na kuendelea kujiimarisha kileleni. Ferguson pia amefurahi kwani hakuna
mchezaji wa Man utd hata mmoja aliyeumia kwenye international game zilizochezwa
wiki hii. Sir Alex alisema “Kwasasa kikosi changu kipo full, nina wigo mpana wa kuchagua
wachezaji watakaocheza”. Man utd wikiendi hii itacheza na Sunderland
siku ya jumamosi na jumatatu itakuwa darajani kucheza na Chelsea kwenye FA cup.
No comments:
Post a Comment