England, Italy, France, German na Spain ni nchi zenye ligi
maarufu sana duniani kwa kuwa na mashabiki wengi. Tathimini ya ligi hizi kwa
mwaka huu imeonesha washindi watapatikana mapema zaidi kabla ya ligi kwisha.
Tukianzia England, Man utd anaongoza kwa tofauti ya point 15 dhidi ya Man City
ambaye anashikilia nafasi ya pili. La Liga, ligi ya Spain, Barcelona anaongoza
kwa tofauti ya point 13 dhidi ya Real Madrid, wakati nchini Italy Juventus
anaongoza kwa tofauti ya pointi 9 dhidi ya Napoli. Nchini Germany kwenye
Bundes, timu ya Bayern Munich imeshaanza kujiandaa kusherekea ubingwa ikiwa na
tofauti ya pointi 20 dhidi ya Dortmund ambaye anashikilia nafasi ya pili, na nchini France PSG pia inaongoza kwa tofauti ya pointi 8
dhidi ya Lyon. Ligi zote zipo ukingoni kwasasa na muda wowote kuanzia wiki ijao
washindi wataanza kutangazwa kabla ya ligi kwisha. Ligi hizi zitaendelea tena wikiendi hii kwenye viwanja tofauti barani
ulaya baada ya international break.
No comments:
Post a Comment