FIFA imeanza kuitambua vyema
Tanzania baada ya kichapo ilichotoa kwa Morocco, hali hiyo imejionesha baada ya
FIFA kuirusha hewani Tanzania kupitia official website yake kama inavyooneka
kwenye picha. FIFA imesema kiwango cha soka la Tanzania kimependa sana kutokana
na mipango yake mizuri ya kuanza kuwekeza kwenye timu za vijana chini ya miaka
15 na 17. Zaidi, FIFA imemtaja kocha Poulsen kuwa ni moja ya chachu ya
maendeleo ya soka Tanzania baada ya kuijenga vyema timu Taifa Stars na timu ya
vijana chini ya miaka 20. Wikendi iliyopita Taifa Stars iliifunga Morocco goli
tatu kwa moja kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia,matokeo ambayo FIFA
imesema yataipandisha Tanzania kwenye renki za viwango ya FIFA mwezi ujao. Tanzania
oyeeeee!!!!!!
No comments:
Post a Comment