Azam FC ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, huenda wakabaki kuwa wawakilishi pekee wa ukanda wa Afrika mashariki baada ya timu nyingi toka ukanda huu zikiwa zimeagamashindano hayo na zile zilizosalia zinasubiri maajabu katika mechi zinazochezwa leo. Timu ya Azam FC, jana ilifanikiwa kutinga raundi ya mwisho ya 16 bora baada ya kuing’oa Barrack Young Controllers II ya Liberia katika mbio za Kombe la Shirikisho. Azam ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa baada ya Simba na Jamhuri kuagahatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wamevuka kikwazo kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.Kufuatia kuichapa BYC ll 2-1 kule Liberia na jana kwenda sare ya 0-0. Matokeo hayo yanaifanya Azam FC inayonolewa na Kocha Stewart John Hall kuzidi kupeta licha ya kushiriki kwa maraya kwanza michuano ya kimataifa tangu kuasisiwa kwao Juni 24, 2007. Ushindi huo unaifanya Azam kukutana na timu kongwe na Mabingwa wa Afrika mbara mbili mwaka 1985 na 2005 FAR Rabat inayomilikiwa na jeshi la Morocco ambapo mechi ya kwanza itachezwa wiki mbili zijazo kati ya Aprili 19 na21 kabla ya kurudiana kati ya Mei 3 hadi 5.
No comments:
Post a Comment