Kiungo wa timu ya Tanzania na klabu ya Simba Amri Kiemba anatarajiwa kuuzwa nchini Morocco kwenye klabu ya Wydad Ac Casablanca. Hatua ya kumuuza mchezaji huyu kwenye klabu hiyo imekuja baada ya Kiemba kuonesha mchezo mzuri wakati Taifa Stars ilipokuwa ikicheza na Morocco wiki iliyopita na Kiemba kuweza kufunga goli zuri la mbali, goli ambalo lilikuwa la kufutia machozi kwa Stars. Kuthibitisha habari hizi, mwenyekiti wa usajili wa klabu ya Simba Hans Pope amekiri kuwa klabu ya Simba imepokea maombi ya klabu hiyo ya Morocco kutaka kumsajili Kiemba na kwasasa wapo kwenye hatua za mwisho kufanikisha uhamisho huo. Kiemba atakuwa mchezaji watatu wa timu ya taifa kucheza nje ya nchi kwenye klabu kubwa barani Afrika baada ya Samatta na Ulimwengu ambao wote wapo TP Mazembe ya Congo DRC. |
No comments:
Post a Comment