Timu ya Azam na AS FAR ya Morocco leo wametoka droo ya bila kufungana katika mechi iliyofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Katika mchezo wa leo Azam walionekana kushindwa kabisa kuingia kwenye ngome ya wapinzani wao ambayo ilionekana kuwa imara zaidi. Azam FC wakiongozwa na John Bocco walijaribu kupangua ngome ya AS FAR na kupiga mashuti ya mbali lakini ngome ya wapinzani wao ilikuwa imara kuhimili mikiki ya Azam hivyo hadi mwisho wa mchezo Azam 0 - 0 AS FAR. Kwa matokeo haya Azam imejiweka katika nafasi ngumu ya kuendelea katika michuano hii kwani italazimika kushinda au kutoka droo ya magoli ugenini ili kusonga mbele katika mchezo unaotarajiwa kufanyika wiki chache zijazo.
No comments:
Post a Comment