Beki mkongwe wa Chelsea John Terry jana alishangaza watu
baada ya kugoma kumpa mkono mwenyekiti wa shirikisho la mpira la Uingereza
bwana David Bernstein. Terry alifanya kitendo hicho kwenye siku ya makabidhiano
ya kombe la UEFA kwenye ukumbi wa Banqueting jijini London. Terry na wachezaji
wenzake wa Chelsea Lampard, Torres na Cech walikuwa wamepanga mstari kwa
kusimama wakiwakaribisha wageni rasmi ambao ni waziri wa michezo wa England,
raisi wa UEFA, meya wa London na mwenyekiti wa FA, wageni hawa kabla ya
kukabidhiwa kombe na Chelsea walianza kwa kusalimiana ambapo mbele ya umati
wote uliofurika kwenye ukumbi ukiongozwa na waziri wa michezo pamoja na raisi
wa UEFA Michael Platini, John Terry aligoma kumpa mkono Bwana David Bernstein
jambo ambalo lilimfanya Bernstein ajisikie aibu sana. Katika maelezo yake
baada ya kutoka nje wa ukumbi John Terry alisema “nisingeweza kumpa mkono
kwasababu kitendo alichonifanyia hakikuwa cha haki, yeye ndiye mbele kwenda
mahakamani kuelezea kesi yangu na Anton Ferdinand”. Alipohojiwa bwana Bernstein
kuhusiana na jambo hilo alisema “mimi siwezi kuongelea maswala ya kijinga, ila
ni kweli mimi na Terry hatuna mahusiano mazuri tokea kesi yake itolewe hukumu”.
John Terry mwaka jana alimfanyia kitendo cha kibaguzi mchezaji wa QPR Aston
Ferdinand, kwa kitendo hicho alifungiwa kucheza mechi tano pamoja na kulipa faini
ya paundi laki 220,000 jambo ambalo linamuuma John Terry hadi leo.
Bernstein mwenyekiti wa FA akitabasamu kwa aibu huku akisalimiana na wachezaji wengine wa Chelsea baada ya kuchuniwa na John Terry aliyekuwa mbele ya mstari. |
No comments:
Post a Comment