Kocha msaidizi wa Simba Julio amepokea kichapo kwa kupigwa ngumi ya jicho na mchezaji wa Toto ya Mwanza Emanuel Sita.Kisa kinasemekana ni kudaiwa kuwa mchezaji wa Toto aliiba mpira unaosemekana ni wa Simba ndipo vurugu ilipoanza na hatimaye Sita kumpiga ngumi ya jicho kocha msaidizi wa Simba. Hata hivyo Julio ameapa kupitia vyombo vya habari kwamba atalipiza kisasi kwa gharama yoyote dhidi ya mchezaji huyo licha ya kuwa hakueleza atalipiza vipi. Jumamosi iliyopita Simba walikuwa jijini Mwanza wakicheza na Toto katika mchezo wa ligi kuu ulioisha kwa droo ya goli moja moja.
No comments:
Post a Comment