Mbio za Jumapili Aprili 21 za marathon
jijini London zinaandaliwa huku kukiwa na ulinzi mkali ulioimarishwa kufuatia mashambulizi ya bomu yaliyozikumba mbio za marathon
za Boston nchini Marekani jumatatu ya wiki hii. Milipuko hiyo miwili ambayo iliwauwa watu watatu na
kuwajeruhi wengi mjini Boston, imewalazimu
waandalizi wa mbio za London kuimarisha mikakati ya usalama katika jitihada za
kuwapa matumaini wanariadha pamoja na watazamaji wanaokadiriwa kufikia nusu milioni watakaojitokeza
kushangilia mitaani. Mitaa yote itakayotumiwa katika mbio za Marathon za London
imewekwa ulinzi mkali. Vilevile, Wanariadha watavaa vitambaa vyeusi kama kumbukumbu ya wale waliopoteza maisha katika mashambulizi ya Boston na waandalizi wamesema pia Euro mbili na senti thelathini zitatolewa na kila mwanariadha atakayemaliza mbio hizo kugharamia waathiriwa wa mashambulizi ya Boston.
No comments:
Post a Comment