Tuesday, April 2, 2013

Ronaldo atoa ushauri kwa Neymar


Mkongwe Ronaldo de Lima (36) amesema Neymar atafanikiwa zaidi akienda kucheza soka Ulaya kabla ya kombe la dunia mwaka 2014. “kipaji cha Neymar ni kikubwa kuzidi timu aliyopo, anatakiwa kwenda Ulaya akacheze na watu wenye kipaji kama chake, kwasasa anakionea kipaji chake, mazingira aliyopo hayakidhi uwezo wake kabisa” alisema Ronaldo kupitia Sports Spectacular. Neymar mwenye umri wa miaka 21 kwasasa anacheza kwenye club ya Santos nchini Brazil, na amesema hatoweza kuondoka Santos hadi kombe la dunia kupita, licha ya kupata ofa nzuri kutoka kwa Barcelona, Chelsea, PSG na Real Madrid.  

No comments:

Post a Comment