Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam FC katika mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayochezwa kesho (Aprili 20 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Azam FC ina fursa nzuri ya kufanya vizuri kwenye mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Emile Fred kutoka Shelisheli. TFF inatoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuiunga mkono Azam FC ikiwa ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa baada ya Simba kutolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
No comments:
Post a Comment