Makocha wasaidizi wa timu zote mbili Azam FC na AS
FAR wametambiana leo katika press conference juu ya mechi yao itakayofanyika
April 20 uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Kalimangonga Ongala wa Azam FC
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mechi hiyo, alisema
wamejiandaa vya kutosha na wanaahidi Watanzania kuwa wataibuka na ushindi
mnono. Ongala pia alisema katika maandalizi yao walifanikiwa kupata DVD za
mechi tatu za mwisho za AS FAR Rabat, moja ikiwa dhidi ya timu ya Al Nasir ya
Libya ambayo waliitoa katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho na
nyingine mbili za ligi ya Morocco ambazo wamezifanyia kazi. Naye Ouadani
wa AS FAR amesema hawaifahamu vizuri Azam FC, lakini wanaujua mpira wa Tanzania
baada ya kuangalia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa
Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) iliyochezwa jijini Dar es Salaam Machi
24 mwaka huu na Stars kushinda mabao 3-1, kocha huyo amesema kupitia mechi hiyo
ya Tanzania wameweza kujifunza kidogo mtindo wa uchezaji mpira wa Tanzania kitu
ambacho anasema kitawasaidia.
Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi ndani ya uwanja wa Azam Chamanzi jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wao dhidi ya AS FAR |
Azam FC na AS FAR ni timu zenye wachezaji wazuri
ambao wanachezea timu za taifa, wachezaji wa Azam FC waliopo kwenye timu
ya taifa ambao pia wanatarajia kuwepo kwenye mechi ni pamoja na Aishi Manula, Mwadini
Ally, Khamis Mcha, John Bocco na Salum Abubakar wakati AS FAR Rabat ina
wachezaji sita kwenye timu ya Taifa ya Morocco ambao mabeki Younes Bellakhdar,
Abderrahim Achchakir, Younnes Hammal, na viungo Salaheddine Said, Salaheddine
Aqqal na Youssef Kaddioui. Watanzania wanaombwa kujitokeza kwa wingi
kuishangilia Azam FC
Kikosi cha AS FAR kilipokuwa kikiwasili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambao wamefikia kwenye hotel ya Saphirre Kariakoo. |
No comments:
Post a Comment