Klabu ya Man City imetoa ofa kwa mshambuliaji wa Napoli
Edinson Cavani ya paundi milioni 13.3 kama mshahara wake wa mwaka ili akubali
kujiunga na klabu hiyo. Man City wametoa ofa hiyo ikiwa ni kubwa kuliko ya Real
Madrid ili wamvutie Cavani kujiunga na Man City. Cavani akikubali ofa hiyo ya
Man city basi atakuwa ni mchezaji anayelipwa zaidi ya wote kwenye ligi ya
Uingereza licha ya kuwa Cavani mwenyewe anapenda kwenda Real Madrid. Mbali ya Real Madrid na Man City, vilevile Chelsea, PSG na Man Utd
wanamuwinda mshambuliaji huyu akiwa ni mbadala wa Falcao ambaye bado hajaonesha
nia ya kuhama Atletico Madrid. Cavani raia wa Uruguay mwenye umri wa miaka 26 hadi
sasa ameshacheza mechi 29 za ligi na anaongoza kwa ufungaji wa magoli katika
ligi ya Italia akiwa na magoli 22.
No comments:
Post a Comment