Kocha wa Man City Roberto Mancini amekubali matokeo na kukiri kuwa Man utd ni mabingwa baada ya kichapo cha goli tatu kwa moja Man city ilichokipata kutoka kwa Tottenham. 'Ubingwa tulikuwa tunautaka mwaka huu ila mambo yamekuwa magumu, ninachopenda kusema ni 'congratulation Man utd', nikiwa nyumbani nitaangalia mechi yao dhidi ya Aston Villa ili nione wanavyoshangilia, ila Man utd sio timu nzuri kuzidi Man city lakini wanastahili kuwa mabingwa kwasababu sisi tumepoteza michezo ambayo hatukustahili kupoteza, tuna sababu nyingi kwanini hutajaweza kuwa mabingwa ila msimu ujao hatutakuwa tayari kufanya makosa tuliyoyafanya msimu huu, hayo yalikuwa maneno yake Roberto Mancini. Man utd leo inacheza na Aston Villa na kama Man utd itashinda mchezo wa leo itafikisha pointi 84 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote hivyo itatangazwa kuwa mabingwa wa BPL mwaka 2012/2013.
No comments:
Post a Comment