Messi akiwa ameinama akisikiliza maumivu |
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi jana alipata maumivu kwenye paja la mguu wake wa kulia iliyopelekea kupumzika kwenye mechi kati ya PSG na Barcelona, mechi iliyokwisha kwa droo ya goli mbili kwa mbili. Daktari wa Barcelona amesema Messi atafanyiwa uchunguzi pindi atakaporudi Spain ili kugundua tatizo lake. Messi kwa kipindi kirefu alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya misuli ambayo yalimfanya akae nje kwa muda mrefu lakini tokea mwaka 2008 amekuwa fiti kabla ya jana kusumbuliwa tena ila madaktari wa club wamesema sio tatizo kubwa.
No comments:
Post a Comment