Carlos Tevez mshambuliaji wa Man City leo amehukumiwa kwenda
jela miezi sita au kulipa faini ya paundi 1,145 baada ya kushikwa na polisi
akiendesha gari bila insurance. Carlos Tevez aliamua kulipa faini ya paundi
1,145 na kutumikia kifungo cha nje kwa kuhudumia jamii kwa masaa 250 ndani ya
miezi 12 ijayo. Tevez pia hatoruhusiwa kuendesha gari kwa kipindi cha miezi
sita na itamlazimu kupewa kibali na mahakama ili aweze kuendesha tena gari
baada ya miezi sita kuisha.
No comments:
Post a Comment