Mbio za kilomita 220 za Jangwa la Sahara ndiyo ngumu kuliko
zote duniani. Mbio hizi zinashirikisha wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50
duniani kote. Mbio za Sahara zinazojulikana kwa jina maarufu “Highway to hell”
hufanyika katika nchi ya Morocco kila mwaka ikishirikisha wakiambiaji zaidi ya
1,000 wakike kwa wakiume. Ugumu wa mbio hizi, wakimbiaji wanatakiwa kukimbia
kwa kilomita 220 kwa kutumia siku saba.
Mbio hizi zina historia ya kusababisha
vifo vya watu watatu kutokana na hali mbaya ya hewa inayofikia digrii 50
zikiambatana na vumbi zito lenye upepo na jua kali. Sheria za mchezo huu kila
mshiriki anatakiwa kukimbia bila kupumzika kilomita 75 kwa masaa 34, akiwa
amebeba chakula, maji na baadhi ya vifaa vya kumsaidia kukimbia visivyopungua kilo tano.
Washiriki wa mbio za Sahara
wakikatisha kwenye jangwa kukiwa na jua kali, upepo na joto lililofika digrii
50
|
Mshiriki akikatisha kwenye vilima vidogo vidogo vyenye mchanga
mzito
|
Washiriki wakipandisha mojawapo ya mlima mrefu katika mbio hizo
|
No comments:
Post a Comment