Mshambuliaji wa Ac Milan Mario Balotelli wikiendi hii
ameshikwa na wasimamizi wa treni akiwa kwenye choo cha treni anavuta sigara.
Kampuni ya treni imesema itampiga faini kwa kitendo alichokifanya kwani uvutaji
wa sigara ni marufuku kwenye treni za Italia. Ac Milan walikuwa safarini kwenda
kucheza na FIorentina katika mechi iliyoisha kwa droo ya goli mbili kwa mbili.
Tukiliangalia kwa undani swala la uvutaji wa sigara kwa
mchezaji wa mpira linaonesha dhahiri kuwa Mario Balotelli anaelekea kuharibu
kipaji chake kwasababu uvutaji wa sigara unaleta madhara makubwa kwenye mapafu
ambavyo ni viungo muhimu kwa mwanadamu kumwezesha kuhema/kupumua. Ikumbukwe kuwa
mchezaji yoyote wa michezo ya kutumia nguvu kama soka anahitaji mapafu yenye afya njema ili
kumpatia uwezo wa kustahimili harakati za mpambano ndani ya kiwanja. Lakini kwa
upande wa Balotelli itamchukua muda mfupi kuchoka kucheza soka kwani sigara ina
tabia ya kula kwa kasi mapafu na hata kusababisha kansa ya mapafu kitu ambacho
ni hatarishi kwa ajira yake.
Balotelli akiwa na sigara mkononi |
Wachezaji wengi ndani na nje ya nchiwamepoteza sifa zao na hatimaye
kuachana na soka kabisa kwasababu ya uvutaji wa sigara wakiwemo Johan Cruyff,
Jack Charlton na Jackie Milburn. Johan Cruyff alifikia hatua ya kuvuta sigara
20 kwa siku, kitendo ambacho kilimfanya aachane na soka akiwa na rekodi nzuri
ya kuwa mchezaji bora wa FIFA mara tatu, hii leo Cruyff ni balozi wa kupambana
na uvutaji wa sigara kwa wachezaji. Clubs zote ulaya zinakataza wachezaji kuvuta sigara kwani wanajua kitendo hicho kitawafanya waishiwe mapema, lakini
imekuwa vigumu sana kusimamia sheria hiyo ikiwa sio rahisi kumfuatilia mchezaji
mmoja mmoja hadi anavyoishi nyumbani kwake. Kwasasa wachezaji ambao wameshashikwa mara kadhaa wakivuta sigara ni pamoja na Rooney, Berbatov, Macheda, Balotelli,
Buffon, Nesta na Laquinta. Wachezaji wote hawa uwezo wao
umeshuka sana sababu mojawapo ikiwa ni uvutaji wa sigara kupita kiasi.
No comments:
Post a Comment