Klabu ya Arsenal ipo kwenye hatua za mwisho kumnasa kiungo
wa Fiorentina Stevan Jovetic. Kocha wa Arsenal, Arsene
Wenger amekiri jambo hilo na kusema Arsenal imeshatenga paundi mil 25 kwa ajili
ya Jovetic, na uhamisho wake unangojea ligi kuisha ili kuona kama Arsenal
itashiriki UEFA champions au la, Wenger amesema kama Arsenal itashiriki UEFA champions
mchezaji huyo atasajiliwa haraka lakini Arsenal ikishindwa kuishiriki UEFA basi
mipango itabadilika. Katika kuimarisha kikosi chake, Arsenal wametenga kiasi
cha paundi mil 70 mwishoni mwa msimu ikiwemo kumnasa kipa wa Hamburg Rene Adler
na David Villa. Stevan Jovetic (23) mzaliwa wa Yugoslavia amejiunga na
Fiorentina mwaka 2008 hadi sasa ameshacheza mechi 111 na kufunga magoli 34.
No comments:
Post a Comment