Friday, April 26, 2013

Ujerumani 8-1 Hispania

Wakati Hispania ikiendelea kutafakari kwanini Barca na Real zilifanya vibaya sana dhidi ya wapinzani wa Bundesliga, Bayern na Dortmund, nchini Ujerumani Wajerumani wanaota "Der Klassiker“ yani fainali kati ya Bayern na Dortmund itakayochezwa katika uwanja wa Wembley jijini London mnamo Mei 25. Rais wa shirikisho la soka Ujerumani (DFB) Wolfgang Niersbach amesema Bayern na Dortmund zimedhihirisha kiwango cha juu cha soka la Ujerumani na kwamba Wajerumani kwasasa wanajipanga kwenye Wembley kushangilia fainali ya timu mbili zikiwa zote ni za Ujerumani. Naye kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani "Die Manshaft“ Joachim Löw amesema wachezaji wake 14 waliopo kwenye nusu fainali ya UEFA pamoja na Mesut Ozil na Sami Khedira wa Real Madrid, unakifanya kikosi cha Ujerumani kuimarika zaidi husani katika kipindi hiki cha kuelekea kombe la dunia litakalofanykia nchini Brazil mwakani. Bayern Munich na Dortmund zikiwa zote ni timu za Ujerumani katikati ya wiki hii ziliweza kuibuka na ushindi mnono wa magoli manne dhidi ya wapinzani wao Barcelona na Real Madrid za Uhispania jambo ambalo linajumuishwa kwa kusema Ujerumani 8-1 Uhispania. Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika wiki ijayo ikiwa wapenzi wa soka wanangojea kuziona timu za Ujerumani kusonga mbele. 

No comments:

Post a Comment