Wachezaji watano wa club ya Yanga watakosekana uwanjani kwa
muda wa wiki moja hadi wiki mbili wakiwa majeruhi. Wachezaji hao wametajwa kuwa
ni Jerry Tegete, Stephano Mwasika, Nizar Khalfan, Omega Seme na Said Mohamed. Mwasika
na Nizar wanasumbuliwa na misuli baada ya kuumia kwenye mechi ya Polisi, Omega
na Mohamed wanamatatizo ya paja na Tegete anasumbuliwa na goti. Wachezaji hao
wote wameshaanza matibabu na wanaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment